Wednesday, August 3, 2011
Sunday, February 27, 2011
FAMILIA YA HAYATI BABA WA TAIFA WAIBASHIRIA CHADEMA KUTAWALA NCHI - 2015
Butiama, Mara
27. 02. 2011 - on 12.15
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimebashiriwa kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 na hivyo kuweza kuongoza nchi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 50 ya uhuru.
Ubashiri huo umetolewa jana kijijini Butiama na mmoja wa watoto wa hayati baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bw. Magige Kambarage alipokuwa akitoa shukrani zake kwa viongozi wa CHADEMA waliokuwa wamekwenda kijijini Butiama kudhuru kaburi la hayati baba wa Taifa na kumjulia hali mama Maria Nyerere.
Bw. Kambarage aliwapongeza viongozi wa CHADEMA kwa uamuzi wao wa kuendesha maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima lengo likiwa ni kuzungumzia mstakabali wa Taifa la Tanzania .
Alisema pamoja na kwamba wapo baadhi ya watu wanaogombana katika mambo ya kisiasa lakini watu hao wanasukumwa kufanya hivyo kutokana na ujinga unaowakabili.
“Kugombana ndani ya siasa ni ujinga tu ndiyo unaotusumbua, mimi nasema kitendo hiki cha maandamano mlichokifanya ni kitendo kizuri sana , pamoja na kwamba mimi ni mwanachama wa CCM, lakini nakupongezeni,”
“Hizi safari za kutembea kwa miguu na kushirikiana na wananchi ni kitu muhimu, eleweni kwamba mna dhamana kubwa hivi sasa mbele ya umma wa Tanzania , kwani ninyi ndiyo kambi kuu ya upinzani hapa nchini, fanyeni kazi msije mkapoteza dhamana mliyokabidhiwa na wananchi, umma umeishawakubali,” alieleza Bw. Kambarage.
Alisema katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, watu wengi hawakujitokeza kupiga kura, lakini wapo zaidi ya milioni 20 wenye haki ya kupiga kura, ambapo aliwataka viongozi hao wa CHADEMA wafanye kazi kubwa ya kuwatafuta waliko ili ifikapo mwaka 2015 waweze kupiga kura.
“Mimi nasema hawa ambao hawakupiga kura wapo wengi sana, watafuteni waliko, 2010 CCM tulipata kura milioni tano za urais, lakini naamini mkiwatafuta hawa waliopotea, katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 CHADEMA mtazoa zaidi ya kura milioni sita na CCM tutaambulia kura milioni nne, naamini hivyo,” alieleza Bw. Kambarage.
Alisema moja ya kazi wa vyama vya upinzani nchini ni kuwainua watanzania katika mambo ambayo serikali iliyoko madarakani imeshindwa kuwatekelezea na kwamba hivi sasa watanzania wameisha kikubali chama cha CHADEMA na ndiyo maana wanakiunga mkono badala ya CCM, “…..nakuombeeni mungu aibariki kazi yenu,” alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe alimweleza mama Maria Nyerere kuwa lengo la ziara yao hiyo ni kumjulia hali yeye na familia yake, kudhuru kaburi la hayati baba wa Taifa na kuomba dua katika kaburi lake ikiwa ni katika kuenzi heshima aliyokuwa nayo katika Taifa la Tanzania.
“Nachukua fursa hii kukushukuru kwa heshima kubwa uliyotupatia ya kukubali kuja kukujulia hali pamoja na kuzulu kaburi la hayati baba wa Taifa, tunasema hii ni heshima kubwa kwetu sisi CHADEMA wakati tukiwa katika mkoa wa Mara kuendesha maandamano ya amani na mikutano ya hadhara kuzungumzia mstakabali wa Taifa letu,”
“Tunaomba utuombee kwa mungu ili tuweze kufanya kazi zeru vizuri na ikibidi kutuunga mkono, basi utuunge katika lolote lile ambalo tutahitaji kuungwa mkono na wewe, lengo letu ni moja tu kuwatumikia watanzania ili waweze na wao kufaidi matunda ya uhuru wa nchi yetu,” alieleza Bw. Mbowe.
Kwa upande wake mama Maria Nyerere aliwashukuru viongozi hao wa CHADEMA kwa uamuzi wa kumtembelea ili kumjulia hali ambapo aliwaombea kwa mungu aweze kuwapa afya njema na waendelee kuwatumikia wananchi kwa haki bila ya upendeleo wowote.
Msafara wa viongozi wa CHADEMA ukiongozwa na mwenyekiti wake wa Taifa, Bw. Freeman Mbowe na katibu mkuu wake Dkt. Wilbroad Slaa uliwasili kijijini Butiama saa 6.00 mchana jana na kupokelewa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara Bw. Makongoro Nyerere ambaye ni mmoja wa watoto wa hayati baba wa taifa.
CHADEMA WATINGA BUTIAMA KWA HAYATI BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS NYERERE
MAKONGORO NYERERE, AMBAYE NI MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA AKIWA NA MWENYEKITI WA TAIFA YA CHADEMA, BW. FREEMAN MBOWE PAMOJA NA MAMA MARIA NYERERE WAKIELEKEA KATIKA KABURI LA HAYATI BABA WA TAIFA, MWALIMU NYERERE SIKU AMBAYO VIONGOZI WA CHADEMA TAIFA WALITEMBELEA KIJIJINI BUTIAMA, MKOANI MARA, FEBRUARI 27, 2011.
VIONGOZI WA CHADEMA WAKITOA HESHIMA KATIKA KABURI LA HAYATI MWALIMU NYERERE
VIONGOZI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) WAKITOA HESHIMA ZAO MBELE YA KABURI LA HAYATI BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE, KUTOKA KULIA NI MWENYEKITI WA TAIFA, BW. FREEMAN MBOWE, MAMA MARIA NYERERE, DKT. WILBROAD SLAA, MEYA WA MANISPAA YA MUSOMA, BW. ALEX KASURURA, BW. MAGIGE KAMBARAGE WANANE KUTOKA KULIA NI MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA, BW. MAKONGORO NYERERE, AMBAYE PIA NI MTOTO WA HAYATI MWALIMU NYERERE.
Friday, February 18, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)